Showing posts with label news. Show all posts
Showing posts with label news. Show all posts

Monday, September 23, 2019

UKWELI WA CELINE DION KWA DRAKE

Mwana mama CELINE DION ambaye ni mkongwe na fund wa vibao kama NEW DAY HAS COME, MY HEART WILL GO ON na THE POWER OF LOVE  ameweza kumuomba msanii mwenzake (rappa) DRAKE mkali wa kibao cha GOD PLAN  pindi alivyo kuwa akihojiwa na radio moja nchin CANADA ijulikanayo kama IHEARTRADIO ombi la mwana mama huyo kwa drake ni kumtaka msanii DRAKE asichole tatuu ya sura ya celine dion mwilin mwake na amemtaka akishindwa kabisa basi achole tatuu feki,,, maneno ya CELINE DION yalikuwa hivi(please drake , i,love you very much. Can i tell you something, do not get a tatoo of my face  in you body. Lakin rapa huyo, star wa gods plan ameonekana kutokumjibu chochote mwanamamaCELINE DION


                                                 mawazo ni muhimu,wew unazani kwan celine dion kamuomba drake asifanye ivo na kwann drake alitaka kuchora tatoo ya mwanamama huyo mwili mwake kama alivyo chola ya msani mwenzake LILY WAYNE      unaweza KUKOMENTI na KUSHILIKISHA pia

Sunday, September 22, 2019

WASANII MATAJILI DUNIANI WA HIP HOP


   Jalida maarufu dunia  lijulikanalo kwa jina la Forbes limetoa listi ya wasaniii wa hip hop matajili dunia kwa mwaka 2019,,listi hiyo ikishikiliwa na wasanii watano toka marekai uku ukiongozwa na msanii JAY Z ambaye ndo namba moja akiwa na utajili wa $1billion akifuatiwa na DR.DRE akiwa msanii wa pili akiwa na utajili wa $800 million,Nafasi ya tatu ikienda kwa DIDDY ajulikanae kama muuza magazeti  kwa utajili wa$700 million nafasi ya NNE ikienda kwa KANYE WEST mwenyew utajili wa $240, Na mwisho katika listi ya matajili hao ni msanii DRAKE mwenyew utajili wa $150 million. Hiyo ni listi ya Mwaka 2019 kwa mu

Wednesday, July 31, 2019

WATANZANIA KUITWA TUMBILI< NINI MAON YAKO

Ronald Reagan: Kwa nini rais huyo wa zamani Marekani aliwaita wajumbe wa Tanzania 'tumbili'Aliyekuwa rais wa marekani Renald Reagan

Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan aliwaita tumbili wajumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa UN mwaka 1971 wakati alipokuwa gavana wa Jimbo la California katika ukanda wa sauti uliochapishwa na The Atlantic.
Alitoa matamshi hayo ya kibaguzi katika mawasiliano ya simu kwa aliyekuwa wakati huo rais wa Marekani Richard Nixon ambaye alirekodi simu zake zote.
Gavana huyo alikasirishwa kwamba wajumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa UN hawakuiunga mkono Marekani katika kura ya kuitambua CBaada ya kura hiyo, wajumbe wa Tanzania walikuwa wameanza kucheza densi katika ukumbi wa UN.hina na kuipiga marufuku Taiwan.

Tuesday, July 30, 2019

KUMEKUCHA IRAN NA UINGEREZA >HALI BADO TETE

Grace 1Nahodha wa meli ya mafuta iliyotekwa na ilipokuwa imebeba mafuta ya Iran amesema kuwa Kikosi cha majini cha Uingereza kilitumia "kikosi cha ghasia " katika kuiteka meli.
Mapema wiki hii, Vikosi vya Marekani viliwalazimisha maafisa wa Gibraltar ambao mewli yao ya mafuta ilikuwa imebeba imebeba mafita kuelekea nchini Syria jambo ambalo lilikuwa ni ukiukaji wa vikwazo vya Muungano wa Ulaya.
Nahodha amesema kuwa kikosi cha wanamaji cha Uingereza waliwalazimisha wahudumu wake ambao hawakuwa na silaha kupiga magoti kwa kuonyeshwa mtutu wa bunduki.
Hata hivyo Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema kuwa kutekwa kwa meli hiyo ilikuwa ni kulingana na "sheria na miiko ya kimataifa ".
Tarehe 4 Julai, takriban wanamaji 30 kutoka kikosi cha askari wa uvamizi 42 walisafirishwa kwa ndege kuutoka nchini Uingereza hadi Gibraltar kusaidia kuikamata meli na shehena yake , kufuatia ombi la serikali ya Gibraltar.

MJUE ALIYE PEWA SUMU KWA KOSA LA KUMPINGA RAISI

Alexei Navalny: Ni nani?
Police officers detain Russia's top opposition figure Alexei Navalny (C) after his visit the city's election commission office to submit documents to get registered as a mayoral election candidate in Moscow July 10, 2013.
  • Alizaliwa Juni 4 1976 huko Butyn, katika eneo la Moscow
  • Alihitimu sheria katika chuo kikuu cha Friendship of the Peoples Moscow mnamo 1998
  • Anaishi Moscow na mkewe na wanaw
    Navalny alikamatwa na kuwekwa gerezani kwa siku 15 kufuatia maandamanoya kwanza mnamo Desemba 5 2011 lakini akabuka kuzungumza katika mkutano mkubwa wa kisiasa baada ya uchaguzi Moscow Desemba, uliohudhuriwa na watu 120,000.
    Putin alichaguliwa tena kama rais kwa urahisi na kamati yenye nguvu ya uchunguzi nchini ikaidhinisha uchunguzi dhidi ya shughuli za Navalny za siku za nyuma, kiasi cha hata kuhoji sifa yake ya uwakili.
    Alipokamatwa kwa muda mfupi mnamo Julai 2013 kwa ubadhirifu wa fedha katika mji wa Kirov, hukumu hiyo ya miaka mitano ilitazamwa pakubwa kama ya kisiasa.
    Aliachuliwa huru ghafla kupiga kampeni kwa uchaguzi wa u Meya Moscow, iambapo alipata 27% ya kura nyuma ya mshirika wa Putin, Sergei Sobyanin.
    Huo ulitazamwa kama ufanisi kutokana na kuwa ushindi wake ulitokana na intaneti na kwa kuzungumza na watu pekee.Alexei Navalny returns from Kirov after his 5-year term was made a suspended sentence
    Kesi yake ikageuzwa na mahakama ya juu zaidi Urusi kufuatia uamuzi wa mahakama ya haki za binaadamu ya Ulaya kwamba kesi yake haikusikizwa kwa usawa.
    Alafu katika kusikizwa tena 2017, alishtakiwa kwa mara ya pili na kupewa hukumu ya baadaye ya miaka mitano.
    Alitaja hukumu hyo kama jitihada ya kumzuia kuwania katika uchaguzi mkuu wa 2018.Police officers detain protest leader Alexei Navalny outside Zamoskvoretsky district court in Moscow, on 24 February 2014

    Afya yake sasa

    Madaktari wanamfanyia ukaguzi hivi sasa kubaini chanzo cha kuugua kwake ghafla baada ya kukamatwa hivi karibuni.
    Ripoti za awali zinaashiria alipata mzio mkali zilizochangia uso wake kufura macho kutoka maji na kutokwa na vipele mwilini.
    Hatahivyo, daktari binafsi wa Navalny siku ya Jumapili amesema hajawahi kukabiliwa na mzio katika siku za nyuma na huenda amekumbana na 'kitu chenye sumu'.
    Maafisa wa afya waliomhudumia wanasema walifanikiwa kumtibu Jumatatu, na wamepanga ukaguzi wa kando wa sampuli za nywele zake na fulana aliovaa .

Takwimu zaonyesha 37% ya watoto wilayani Mpwapwa Tanzania wanakosa lishe bora


utapia mloWilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma inaripotiwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wenye tatizo la utapia mlo.
Takwimu rasmi za wilaya hiyo zinaonyesha kuwa asimilia 37 ya watoto elfu sabini waliopo katika eneo hilo, wanakosa lishe bora.
Licha ya huduma na jitihada zinazofanywa kwa sasa na serikali, bado tatizo hilo linaonekana kujikita mizizi.
Kwenye wodi ya watoto katika Hospitali ya wilaya ya Mpwapwa, vitanda kadhaa vina watoto waliolazwa na wazazi wao.
Baadhi ya watoto hao wamelazwa kwa kuathirika kwa utapia mlo kama ilivyo kwa Margaret Ndemunuwinda na mwanawe.
'Tumelazwa hapa tangu Ijumaa, tumbo limejaa gesi alafu alikuwa amevimba usoni na miguuni...mpaka sasa hivi nipo ila bado hajapata nafuu... tatizo sina hela ya kumnunulia lishe' anaeleza Margaret kuhusu hali inayomkabili mwanaye mchanga aliyelazwanaye hospitalini humo.
Renatus Kombo, afisa lishe wilayani Mpwapwa anasema mara nyingi watoto wenye tatizo la utapia mlo, huathirika katika kipindi kama hichi ambacho baadhi ya wazazi wanatumia muda mwingi kuandaa mashamba huku wakiwaacha watoto bila lishe bora.utapia mlo
'Wengine hawafiki katika zahanati kwa wakati' anaeleza Renatus na kuongeza kwamba changamoto ni kubwa ya watu kutoelewa umuhimu wa lishe bora licha ya kwamba vyakula vipo.
'Wanategema sana kwenye (vyakula) vya uwanga. Kama ni ugali wa mtama basi ni ugali wa mtama mwezi mzima. Anasahau kwamba kuna matunda, ubuyu, ila hajui matumizi ya buyu ni nini ila ubuyu una faida kubwa sana. hajui pale nyumbani kuna mayai inabidi ayatumie' anafananua afisa huyo.

Utapia mlo ni nini?

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO hii ni hali inayogusia mapungufu, viwango vya ziada au ukosefu wa usawa wa virutubisho katika chakula anachokula mtu
Takriban watoto milioni 41 walo chni ya miaka mitano duniani wana uzito wa kupitiliza na hiyo ni sehemu ya athari ya ukosefu wa lishe bora, huku wengine milioni 159 wakiathirika ukuwaji kutokana na utapia mlo.
WHO linataja kwamba tatizo linatokana na familia nyingi kutoweza kugharamia chakula au kupata chakula chenye virutubisho vya kutosha kama matunda mboga, maziwa na nyamamtama.
Uelewa mdogo kuhusu lishe bora, umbali wa vituo vya afya na ugumu wa maisha vyote vimeelezwa kuchangia ongezeko la idadi kubwa ya watoto wenye tatizo hilo katika eneo hilo.
Katika ripoti hiyo ya 2018/2019 ya halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, watoto 485 walio chini ya miaka mitano walikuwa na utapiamlo mkali kwa robo ya tatu ya mwaka, na katika robo ya nne, watoto kulishuhudiwa wagonjwa wapya 230, kati yao 167 wametibiwa, wengine wakitoroka matibabu na 4 wakifariki kutokana na kuchelewa kufika kupokea matibabu.
Monica Chibaluo anasema alichelewa kumfikisha mwanawe aliye na miezi kumi hospitalini kutokana na kwamba nyumbani na hospitalini ni mbali.
'Tulikuwa tunatafuta hela ya kuja hospitalini, baba mtoto amemtelekeza, ...lishe hadi uwe una hela, kama karanga, mchele uwe unaweza kununua ili mtoto apate lishe, hizo hela sikuweza kuzipata'.
Kutokana na changamoto hiyo, maafisa wanaeleza kwamba jitihada zimeidhinishwa za kuwawezesha wauguzi kutoa elimu ya lishe bora kwa wananchi ambao wanaishi na tatizo hilo.Baadhi ya jitihada zinazohitajika kuiboresha hali kwa mujibu wa Renatus ni kuhakikisha miundo mbinu ya usafi na maji salama.
Jitihada za kubadili tabia ya watu kwa kutoa elimu na uhamasishaji kupitia mikutano na katika kliniki.
Kadhalika ametaja umuhimu pia kuwajengea uwezo wanaume kufahamu zaidi uzito na maana ya lishe kutokana na kwamba kama mtafutaj, baba ndiye mhusika, 'kama hawezi kutafuta , ina maana familia itaingia katika matatizo'.