Nahodha wa meli ya mafuta iliyotekwa na ilipokuwa imebeba mafuta ya Iran amesema kuwa Kikosi cha majini cha Uingereza kilitumia "kikosi cha ghasia " katika kuiteka meli.
Mapema wiki hii, Vikosi vya Marekani viliwalazimisha maafisa wa Gibraltar ambao mewli yao ya mafuta ilikuwa imebeba imebeba mafita kuelekea nchini Syria jambo ambalo lilikuwa ni ukiukaji wa vikwazo vya Muungano wa Ulaya.
Nahodha amesema kuwa kikosi cha wanamaji cha Uingereza waliwalazimisha wahudumu wake ambao hawakuwa na silaha kupiga magoti kwa kuonyeshwa mtutu wa bunduki.
Hata hivyo Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema kuwa kutekwa kwa meli hiyo ilikuwa ni kulingana na "sheria na miiko ya kimataifa ".
Tarehe 4 Julai, takriban wanamaji 30 kutoka kikosi cha askari wa uvamizi 42 walisafirishwa kwa ndege kuutoka nchini Uingereza hadi Gibraltar kusaidia kuikamata meli na shehena yake , kufuatia ombi la serikali ya Gibraltar.
No comments:
Post a Comment