Monday, July 29, 2019




MASIKINI na UOGA WA MASIKINI
na mwadish wako
Mwaki       29/07/2019





Mtu mmoja aliwahi kusema, "ukichukua fedha zote ulimwenguni na ukizagawa sawa sawa kwa kila mmoja, baada ya mda hela zitawarudia wale walio kuwa nazo mara ya kwanza" Kwanini?

......."Maskini ni watumiaji wakati matajiri ni wawekezaji"......

Nioneshe mtu maskini, nitakuonyesha mtu anae pishana na fursa mara kwa mara.

Mtu anaeona changamoto ndani ya kila fursa badala ya kuona fursa ndani ya kila changamoto.

Kuwa KIJANA sio cheo, ni jukumu. Inamaanisha unapaswa kuwajibika kiuchumi Asubuhi, Mchana na Usiku.

Lazima uchukue maamuzi magumu ili upate matokeo makubwa.

Unapaswa kupanga na kuweka mikakati, lazima uthamini faida na fedha kidogo unayoipata. Lazima uwe makini na mwenye nia kama unataka kufanikiwa.

Watu wanaoshangaza kabisa hapa duniani ni WATU MASKINI.

UMASIKINI Ni kupishana na fursa kila wakati.

Angalia sababu hizi
1) ukiwapa bure, watahisi ni mtego.

2) ukiwaambia ni mradi mdogo wawekeze, watakwambia hauwezi ukaleta faida

3) ukiwambia waingie kuwekeza katika ukubwa, watakwambia sina hela

4)ukiwaambia wajaribu vitu vipya, watakwambia hamna uzoefu: umewahi kuona wapi hichi kitu kimefanikiwa? Nani amewahi kufaidika nacho?

5) Ukiwaambia ni biashara ya kawaida ya kila siku, watakwambia ni kazi ngumu sana hiyo

6) ukimwambia ni mpango biashara mpya, atakwambia mimi huwa siongeagi sana na watu alafu ni kwa miaka mingapi sasa huu mpango biashara umekuwepo?

7) ukimwambia afungue duka, atakwambia nitakosa uhuru ntashindwa kufanya mambo mengine.

8) ukimwambia afate mpango wa biashara yake kwa mwaka mmoja, atakwambia ni mda mrefu sana huo, siwezi subiri.

9) ukimuuliza ni nini anaweza kufanya, atakwambia "naweza kufanya chochote"

10) wanapenda kuwauliza marafiki zao, ambao ni kama wao juu ya mtazamo wao. Hata maandiko matakatifu yameeleza kuwa vipofu, kamwe hawaongozi vipofu wenzao.

11) wanafikiri zaidi ya mkufunzi wa chuo kikuu na wanafanya kidogo kuliko kipofu.

12)Akienda kanisani anasema hana kabisa sadaka lakini wakati huo huo anatoka na kununua maandalizi (ANAAMUA KU'INVEST CHOONI KULIKO KWENYE UFALME WA MUNGU)

Changamoto kubwa sana watu maskini walio nayo, ni kukosa kuchukua hatua

Wanafurahia kasehemu kasiko na mahangaiko. Wanakwea katika dimbwi la ulimwengu wao na ufahamu wao ....

NB;
kuna hatari katika kuchukua hatua, lakini ni hatari zaidi kutokuchukua hatua.. je Ni Bora kuchuka hatua badae usipofanikiwa ukajifunza kitu Katika maisha ya utaftaji? au ukaacha kuichukua hatua badae ukaanza kushangaa mafanikio ya wale waliochukua hatua? (utasikia huyu nilisoma nae secondary) "maneno ya wasiopenda kuchuka hatu"

Bora kuchukua hatua.

Masikin chukua hatua kwa lengo la kukifanya kizazi chako kutoka na kutokuja kuishi kiumasikin kama ilivyo kuwa kwa wew .wekeza shilingi moja ili kesho update shilingi mbili ambazo zitakuwa mlango wa mafanikio kwa kizazi chako

No comments:

Post a Comment