Alexei Navalny: Ni nani?
- Alizaliwa Juni 4 1976 huko Butyn, katika eneo la Moscow
- Alihitimu sheria katika chuo kikuu cha Friendship of the Peoples Moscow mnamo 1998
- Anaishi Moscow na mkewe na wanawNavalny alikamatwa na kuwekwa gerezani kwa siku 15 kufuatia maandamanoya kwanza mnamo Desemba 5 2011 lakini akabuka kuzungumza katika mkutano mkubwa wa kisiasa baada ya uchaguzi Moscow Desemba, uliohudhuriwa na watu 120,000.Putin alichaguliwa tena kama rais kwa urahisi na kamati yenye nguvu ya uchunguzi nchini ikaidhinisha uchunguzi dhidi ya shughuli za Navalny za siku za nyuma, kiasi cha hata kuhoji sifa yake ya uwakili.Alipokamatwa kwa muda mfupi mnamo Julai 2013 kwa ubadhirifu wa fedha katika mji wa Kirov, hukumu hiyo ya miaka mitano ilitazamwa pakubwa kama ya kisiasa.Aliachuliwa huru ghafla kupiga kampeni kwa uchaguzi wa u Meya Moscow, iambapo alipata 27% ya kura nyuma ya mshirika wa Putin, Sergei Sobyanin.Huo ulitazamwa kama ufanisi kutokana na kuwa ushindi wake ulitokana na intaneti na kwa kuzungumza na watu pekee.Kesi yake ikageuzwa na mahakama ya juu zaidi Urusi kufuatia uamuzi wa mahakama ya haki za binaadamu ya Ulaya kwamba kesi yake haikusikizwa kwa usawa.Alafu katika kusikizwa tena 2017, alishtakiwa kwa mara ya pili na kupewa hukumu ya baadaye ya miaka mitano.Alitaja hukumu hyo kama jitihada ya kumzuia kuwania katika uchaguzi mkuu wa 2018.
Afya yake sasa
Madaktari wanamfanyia ukaguzi hivi sasa kubaini chanzo cha kuugua kwake ghafla baada ya kukamatwa hivi karibuni.Ripoti za awali zinaashiria alipata mzio mkali zilizochangia uso wake kufura macho kutoka maji na kutokwa na vipele mwilini.Hatahivyo, daktari binafsi wa Navalny siku ya Jumapili amesema hajawahi kukabiliwa na mzio katika siku za nyuma na huenda amekumbana na 'kitu chenye sumu'.Maafisa wa afya waliomhudumia wanasema walifanikiwa kumtibu Jumatatu, na wamepanga ukaguzi wa kando wa sampuli za nywele zake na fulana aliovaa .
No comments:
Post a Comment